價格:免費
更新日期:2019-06-07
檔案大小:5.5M
目前版本:3.97
版本需求:Android 4.2 以上版本
官方網站:http://onimas.jfp.co.tz
Email:support@jfp.co.tz
聯絡地址:SOKOINE GROUNDS, Mbeya, Tanzania
This is a computer program (system) functioned in English and swahili, that has been developed so as to as analyze, manage business and inventory operations such as expiry, movements and trends of items, manage costs, calculate cashes, analyze extra revenues and expenditures, prepare, examine, and analyze accounting records, financial statements, and other financial reports to assess accuracy, completeness, and conformance to reporting and procedural standards.
Other tasks are storing all stakeholders (customers, vendors and employees) information and details such as customer orders, invoices, balances, etc.
ONIMAS ni program inayochanganua,kuendesha na kumpa mwongozo mfanya biashara katika shughuli zake za kibiashara.
Ni kwa biashara ndogo ndogo (Rejareja) na za maduka ya jumla.
Kwa kutumia ONIMAS mfanya biashara anaweza kujua mzunguko wa fedha, bidhaa, faida iliyopatikana kwa kila bidhaa akiwa mahali popote mfano nje ya eneo la biashara,nje ya mkoa au nje ya nchi.
Pia unaweza kutumia bila mtandao(offline)
KAZI ZINAZOFANYWA NA ONIMAS
i. Kusaidia kudhibiti gharama, kukokotoa fedha
taslimu, kutoa mchanganuo wa mapato na
matumizi ya ziada na kutengeneza ripoti za
faida na hasara za (siku, juma, mwezi, mwaka)
ii. Inatengeneza stock ya bidhaa ya kila siku.
iii. Kumbukumbu za madeni, invoisi, orders kwa
wateja na wasambazaji (vendors).
iv. Kutambua bidhaa zikikaribia mwisho wa muda
wa matumizi (to expire).
v. Kuandaa na kuchambua kumbukumbu za
kifedha (Financial/Accounting records)
vi. Ripoti nyingine ni za mzunguko wa bidhaa
(Stock transfer), mauzo na manunuzi, invoisi,
orders, madeni, taarifa za wafanyakazi, n.k
WATUMIAJI, NI MADUKA YA
i. Vifaa vya ujenzi
ii. Vifaa vya umeme
iii. Vifaa vya mashine (spares)
iv. Vifaa vya nyumbani na shamba
v. Vifaa vya elektroni
vi. Nguo, viatu ,mitumba, n.k
vii. Wauza nafaka, matunda, mboga,
viii. Maduka ya jumla na
supermarket
ix. Wauza mbao, matofali, n.k
x. Wauza vitabu na Stationary
xi. Bidhaa mchanganyiko
xii. Bidhaa za kilimo, mifugo na
madawa
xiii. Vituo vya uzalishaji mikate,
vinywaji, n.k
MAHITAJI KWA ONIMAS YA KOPYUTA
Uwe na kompyuta angalau moja hata yenye uwezo wa kawaida. Inaweza kuwa ya mezani
(desktop) au mpakato (laptop).
KUMBUKA:
Utunzaji wa kumbukumbu katika biashara ni swala la muhimu ili kujua kiasi cha fedha (mali)
kilichopokelewa na kutumiwa kutokana na shughuli za biashara za kila siku.
Haiwezekani kuyakumbuka matukio yote ya juma, mwezi au mwaka katika biashara yako bila
kufanya marejeo kwenye kumbukumbu. Ni kwa kupitia kumbukumbu utaweza kufahamu
mwenendo wa biashara.
Kadri biashara yako inavyokua na idadi ya shughuli za kibiashara zinavyoongezeka, inakuwa
vigumu kufuatilia manunuzi, mauzo, mali, fedha taslimu, wadai na wadaiwa, hivyo kuna
umuhimu wa kuwa na kumbukumbu za biashara ambazo zipo katika mpangilio unaokuwezesha
kujua kwa urahisi mwenendo wa biashara yako.
Wajasiriamali wanapaswa kufahamu kuwa, maamuzi mazuri ya biashara yanatokana na taarifa
toka kwenye kumbukumbu sahihi za biashara. Kumbukumbu zinavyokuwa sahihi ndivyo
ambavyo maamuzi ya biashara yanavyokuwa mazuri zaidi.
Ili kuwa na maamuzi sahihi ya biashara yako, ONIMAS imetengenezwa ili kukusaidia wewe
mfanyabiashara.